Hamia kwenye habari

MEI 13, 2021
URUSI

Mahakama ya Urusi Yakataa Rufaa ya Dada Yuliya Kaganovich

Mahakama ya Urusi Yakataa Rufaa ya Dada Yuliya Kaganovich

Mei 13, 2021, Mahakama ya Eneo Lililotengewa Wayahudi imekataa rufaa ya Dada Yuliya Kaganovich. Badala yake mahakama ya Urusi imeunga mkono ombi la kubadili hukumu ya awali ya Yuliya, ya faini ya rubo 10,000 (dola 135 za Marekani), na kuwa kifungo cha nje cha miaka miwili na miezi sita. Hatahitaji kwenda gerezani wakati huu.