Hamia kwenye habari

MEI 31, 2021
URUSI

Mahakama ya Urusi Yakataa Rufaa ya Mashahidi Wanne

Mahakama ya Urusi Yakataa Rufaa ya Mashahidi Wanne

Mei 28, 2021, Mahakama ya Mkoa wa Omsk ilikataa rufaa ya Ndugu Sergey Polyakov na mke wake, Anastasia, na pia ya Dada Gaukhar Bektemirova na Dada Dinara Dyusekeyeva. Ni lazima Ndugu Polyakov akae gerezani, na dada hao watatu wataendelea na vifungo vyao vya nje.