Hamia kwenye habari

MACHI 2, 2021
URUSI

Mahakama ya Urusi Yakataa Rufaa ya Ndugu Ruslan Alyev

Mahakama ya Urusi Yakataa Rufaa ya Ndugu Ruslan Alyev

HABARI ZA KARIBUNI | Mahakama ya Kuchunguza Upya Maamuzi ya Mahakama za Chini ya Urusi Yakataa Rufaa ya Pili ya Ndugu Ruslan Alyev

Novemba 24, 2021, Mahakama ya Nne ya Kuchunguza Upya Maamuzi ya Mahakama za Chini ilitupilia mbali rufaa ya pili ya Ruslan Alyev na kuunga mkono kifungo cha nyumbani cha miaka miwili na nusu alichokuwa amepewa. Hahitaji kwenda gerezani.

Machi 1, 2021, Mahakama ya Eneo la Rostov ilikataa rufaa ya Ndugu Ruslan Alyev na kuunga mkono kwamba ahukumiwe kifungo cha nyumbani cha miaka miwili na nusu. Hatahitaji kwenda gerezani wakati huu.