Hamia kwenye habari

JUNI 23, 2020
URUSI

Mahakama ya Urusi Yakubali Kumwachilia Dennis Christensen Mapema

Mahakama ya Urusi Yakubali Kumwachilia Dennis Christensen Mapema

Juni 23, 2020, Mahakama ya Wilaya ya Lgovskiy katika Eneo la Kursk ilikubali kumwachilia mapema Ndugu Dennis Christensen. Kupatana na ombi la mwendesha-mashtaka, hakimu alibadili kifungo kilichosalia cha Ndugu Christensen kuwa faini ya rubo 400,000 (dola 5,759 za Marekani). Uamuzi huo utaanza kutenda baada ya siku kumi, wakati ambapo ataweza kurudi nyumbani kwa mke wake, familia yake, na waabudu wenzake. Sifa zote zinamwendea Yehova!