Hamia kwenye habari

JANUARI 26, 2021
URUSI

Mahakama ya Urusi Yamhukumu Dada Galina Parkova Kifungo cha Nje

Mahakama ya Urusi Yamhukumu Dada Galina Parkova Kifungo cha Nje

Januari 26, 2021, Mahakama ya Wilaya ya Leninskiy huko Rostov-on-Don ilimhukumu Dada Galina Parkova kifungo cha nje cha miaka miwili na miezi mitatu. Hatahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Katika maelezo yake ya mwisho mahakamani, alisema hivi kwa ujasiri: “Kwa kuwa nina imani, ninaelewa kwa nini ninapatwa na matatizo haya leo. Bwana wangu Yesu Kristo alitabiri sababu itakayofanya nipatwe nayo. Katika Injili ya Yohana sura ya 15, mstari wa 20, Yesu alisema hivi: ‘Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake. Ikiwa wamenitesa mimi, watawatesa ninyi pia.’

“Ikiwa walimtendea Yesu kwa njia kama hii, ambaye aliwaponya, kuwalisha, na kuwaambia watu kuhusu Baba yake na Ufalme wake wa wakati ujao, basi wafuasi wa Yesu watazamie nini kingine? Kuteswa kwa sababu ya imani yangu kumeimarisha sana usadikisho wangu kwamba niko kwenye njia inayofaa!”