Hamia kwenye habari

FEBRUARI 3, 2021
URUSI

Mahakama ya Urusi Yamhukumu Ndugu Artur Lokhvitskiy Kifungo cha Nje

Mahakama ya Urusi Yamhukumu Ndugu Artur Lokhvitskiy Kifungo cha Nje

Februari 2, 2021, Mahakama ya Wilaya ya Birobidzhan iliyo katika Eneo Lililotengewa Wayahudi ilimhukumu Artur Lokhvitskiy mwenye umri wa miaka 35. Mahakama hiyo ilimhukumu kifungo cha nje cha miaka miwili na miezi sita na miaka mitatu chini ya usimamizi ili kumchunguza tabia. Artur hatahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Katika maelezo yake ya mwisho, Artur alisema hivi: “Ni pendeleo kubwa kushiriki katika shughuli hizi za kihukumu, bila kujali uamuzi utakuwa upi. Kwa mara nyingine nimejionea utimizo wa maneno ya Yesu Kristo. Maneno hayo yanapatikana katika kitabu cha Biblia cha Marko sura ya 13, mstari wa 9 na 10: ‘Lakini ninyi jihadharini. Watu watawapeleka mahakamani, . . . ili kuwa ushahidi kwao. Pia, katika mataifa yote, lazima habari njema ihubiriwe kwanza.’ . . . Kujua jambo hilo kunanichochea kuwaeleza wengine kuhusu makusudi ya Mungu. Ni pendeleo langu kukueleza kuyahusu, Mheshimiwa.”