Hamia kwenye habari

FEBRUARI 12, 2021
URUSI

Mahakama ya Urusi Yamhukumu Ndugu Igor Tsarev Kifungo cha Nje

Mahakama ya Urusi Yamhukumu Ndugu Igor Tsarev Kifungo cha Nje

TAARIFA YA HABARI | Mahakama ya Urusi Yakataa Ombi la Rufaa la Ndugu Igor Tsarev

Aprili 29, 2021, Mahakama ya Eneo Lililotengewa Wayahudi iliunga mkono uamuzi wa kumhukumu Ndugu Igor Tsarev kifungo cha nje cha miaka miwili na nusu alichokuwa amehukumiwa awali. Hatahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Februari 12, 2021, Mahakama ya Wilaya ya Birobidzhan katika eneo Lililotengewa Wayahudi, ilitoa uamuzi wake dhidi ya Ndugu Igor Tsarev. Mahakama ilitoa hukumu ya kifungo cha nje cha miaka miwili na nusu. Igor hatahitaji kwenda gerezani kwa sasa.

Igor aliendelea kubaki imara na kuwa na mtazamo mzuri wakati wote wa kesi yake. Alisema hivi alipotoa maelezo yake ya mwisho mahakamani Februari 11, 2021: “Nilitafakari kuhusu utangulizi wa maelezo yangu ya mwisho mbele ya mahakama, nami nikaamua kufuata ushauri wa mtume Paulo kwa Wakristo wote. Katika barua yake kwa Wakolosai, aliwasihi hivi: ‘Mjionyeshe kuwa wenye shukrani.’

“Hivyo, ningependa kukushukuru wewe, Mheshimiwa, kwa kuwezesha kuwa na mazingira tulivu wakati wote wa kesi, na kwa kutusikiliza kwa makini. .  . . Lakini ninamshukuru sana Muumba na Mungu wetu, kwa sababu amenitegemeza pindi yote kesi ilipokuwa ikisikilizwa. Amenipatia utulivu na amani ya moyo.”—Wakolosai 3:15.