Hamia kwenye habari

Ndugu Khasan Kogut akiwa pamoja na mke wake, Yekaterina baada ya kuhukumiwa

SEPTEMBA 10, 2020
URUSI

Mahakama ya Urusi Yamhukumu Ndugu Khasan Kogut

Mahakama ya Urusi Yamhukumu Ndugu Khasan Kogut

Septemba 10, 2020, Mahakama ya Jiji la Berezovsky katika Eneo la Kemerovo ilimhukumu Ndugu Khasan Kogut. Alihukumiwa kifungo cha nje cha miaka miwili na nusu. Ndugu Kogut anafurahi kwamba hatafungwa gerezani na anaweza kuendelea kuishi na mke wake na mwana wao mwenye umri wa miaka nane.