DESEMBA 22, 2020
URUSI
Mahakama ya Urusi Yamhukumu Ndugu Semyon Baybak Kifungo cha Nje
Desemba 21, 2020, Mahakama ya Wilaya ya Leninskiy huko Rostov-on-Don ilimhukumu Ndugu Semyon Baybak kifungo cha nje cha miaka mitatu na nusu. Hatafungwa gerezani kwa sasa.
Mapema, wakati wa maelezo yake ya mwisho mahakamani, Ndugu Semyon alimnukuu mtetezi wa haki za kibinadamu anayejulikana sana nchini Urusi aliyesema hivi: “Wao [Mashahidi wa Yehova] wanateswa, lakini wanatabasamu.” Kisha Semyon akasema hivi kwa usadikisho: “Hilo ni kweli kabisa. Sijakata tamaa wala sina chuki.” Kisha akasoma andiko la 2 Wakorintho 4:8, 9, na kusema linamhusu yeye na Mashahidi wenzake nchini Urusi: “Tunakandamizwa katika kila njia, lakini hatubanwi kupita kiasi cha kushindwa kusonga; tunafadhaishwa, lakini si bila njia ya kutokea kabisa; tunateswa, lakini hatuachwi bila msaada; tunaangushwa chini, lakini hatuangamizwi.”