Hamia kwenye habari

FEBRUARI 17, 2021
URUSI

Mahakama ya Urusi Yampata na Hatia Dada Yelena Reyno-Chernyshova na Kumtoza Faini kwa Sababu ya Imani Yake

Mahakama ya Urusi Yampata na Hatia Dada Yelena Reyno-Chernyshova na Kumtoza Faini kwa Sababu ya Imani Yake

Februari 17, 2021, Mahakama ya Wilaya ya Birobidzhan katika Eneo Lililotengewa Wayahudi ilitoa uamuzi kwamba Dada Yelena Reyno-Chernyshova ana hatia ya “kushiriki katika utendaji wa shirika lenye msimamo mkali.” Alitozwa faini ya rubo 10,000 (dola 135 za Marekani).