Hamia kwenye habari

Ndugu Aleksey Metsger, ahukumiwa na kupigwa faini na Mahakama ya Urusi kwa sababu ya kutenda kulingana na imani yake

NOVEMBA 21, 2019
URUSI

Mahakama ya Urusi Yampiga Faini ya Rubo 350,000 Ndugu Aleksey Metsger, Yakataa Ombi la Mwendesha-Mashtaka la Kutaka Afungwe Miaka Mitatu Gerezani

Mahakama ya Urusi Yampiga Faini ya Rubo 350,000 Ndugu Aleksey Metsger, Yakataa Ombi la Mwendesha-Mashtaka la Kutaka Afungwe Miaka Mitatu Gerezani

Alhamisi, Novemba 14, 2019, Mahakama ya Wilaya ya Perm, Ordzhonikidzevskiy ilimhukumu Ndugu Aleksey Metsger na kumtoza faini ya rubo 350,000 (dola 5,460 hivi za Marekani). Yeye ndiye ndugu wa 12 nchini Urusi mwaka huu kuhukumiwa isivyo haki kwa kosa la kuwa na msimamo mkali kwa sababu ya kuwaambia wengine na kutenda kulingana na imani yake kwa amani. Wakili wa Ndugu Metsger atakata rufaa uamuzi huu.

Aprili 25, 2019, kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Ndugu Metsger kwa sababu alisema yeye ni Shahidi wa Yehova. Ushahidi uliotumika dhidi yake ulitia ndani mazungumzo ya kidini kati yake na watu fulani waliorekodi mazungumzo hayo kisiri.

Kesi yake ilianza Oktoba 14, 2019. Mwendesha-mashtaka wa jiji alipendekeza Ndugu Metsger ahukumiwe miaka mitatu gerezani. Ingawa mahakama haikuagiza afungwe gerezani, ilimpata kuwa na hatia na kumhukumu. Hilo linasikitisha kwa sababu tabia hiyo itafanya ndugu na dada zetu wengine washtakiwe kwa sababu ya imani yao.

Licha ya kwamba wenye mamlaka wanaendelea kuwatesa ndugu zetu nchini Urusi bila sababu, tunajua kwamba Yehova ataendelea kuwafariji na kuwaimarisha.—Zaburi 119:76, 161.