Hamia kwenye habari

FEBRUARI 15, 2021
URUSI

Mahakama ya Urusi Yamtoza Faini Dada Svetlana Monis kwa Sababu ya Imani Yake

Mahakama ya Urusi Yamtoza Faini Dada Svetlana Monis kwa Sababu ya Imani Yake

Februari 15, 2021, Mahakama ya Wilaya ya Birobidzhan katika Eneo Lililotengewa Wayahudi imempata Dada Svetlana Monis na hatia ya kushiriki katika shughuli za shirika lililopigwa marufuku. Mahakama ilimtoza faini ya rubo 10,000 (dola 135 za Marekani).

Katika maelezo yake ya mwisho mbele ya mahakama, Svetlana alikuwa na imani na ujasiri. Alisema hivi: “Ningependa kuijulisha mahakama kwamba ninasimama mbele yenu . . . kwa sababu ya jina la Bwana wetu, Yesu Kristo, na Baba yake, Yehova Mungu. Biblia inasema hivi kuhusu hilo. 1 Petro 4:14-16 inasema hivi: ‘Ikiwa mnashutumiwa kwa ajili ya jina la Kristo, ninyi ni wenye furaha, kwa sababu roho ya utukufu, yaani roho ya Mungu, inatulia juu yenu. Hata hivyo, yeyote kati yenu asiteseke kwa sababu yeye ni muuaji au mwizi au mkosaji au mtu anayejiingiza katika mambo ya watu wengine. Lakini yeyote akiteseka kwa sababu ni Mkristo, asione aibu, bali na aendelee kumtukuza Mungu huku akilibeba jina hili.’”