Hamia kwenye habari

Ndugu Anatoliy Tokarev akiwa nje ya mahakama mnamo Agosti 2020

OKTOBA 23, 2020
URUSI

Mahakama ya Urusi Yamtoza Faini Ndugu Anatoliy Tokarev

Mahakama ya Urusi Yamtoza Faini Ndugu Anatoliy Tokarev

Oktoba 23, 2020, Mahakama ya Wilaya ya Oktyabrsky huko Kirov ilimhukumu Ndugu Anatoliy Tokarev na kumpiga faini ya rubo 500,000 (au dola 6,552 hivi za Marekani). Ana siku kumi za kukata rufaa uamuzi huo.

Alipotoa maelezo yake ya mwisho mahakamani, Ndugu Tokarev alisema hivi kwa ujasiri: “Wakati wa kesi hii ya uhalifu dhidi yangu, maofisa wa usalama walikuwa wakiniambia: ‘Ama ukane imani yako, au . . . utaadhibiwa vibaya sana mbele ya watu.’ . . . Mheshimiwa, nilisema siku ya kwanza kesi yangu ilipoanza kusikilizwa na nitasema tena sasa, sitakana imani yangu katika Mungu. . . . Ni kweli kwamba vitisho vya kufungwa gerezani au hata kuuawa vinaniogopesha, kama vinavyoweza kumwogopesha Shahidi yeyote wa Yehova. Na wenye mamlaka wanaposema kwamba mimi ni mwenye msimamo mkali wananichafulia jina bila sababu yoyote. Licha ya hayo, Mheshimiwa, siwezi kumwacha Mungu na kukosa upendo wake.”