Hamia kwenye habari

APRILI 2, 2021
URUSI

Mahakama ya Urusi Yapiga Marufuku Programu ya JW Library

Mahakama ya Urusi Yapiga Marufuku Programu ya JW Library

Machi 31, 2021, Mahakama ya Wilaya ya Oktyabrskiy iliyoko St. Petersburg ilitangaza kwamba ’’JW Library’’ ni programu yenye msimamo mkali na ikapiga marufuku isitumiwe katika eneo lote la Shirikisho la Urusi na Crimea. Marufuku hiyo imeanza kutumika mara moja. Watumiaji wameanza kupata matatizo ya kufungua programu hiyo. Rufaa itakatwa dhidi ya uamuzi huo.