NOVEMBA 30, 2020
URUSI
Mahakama ya Urusi Yatoa Hukumu Dhidi ya Mashahidi Wanne, Mmoja Afungwa Gerezani
Novemba 30, 2020, Mahakama ya Wilaya ya Pervomayskiy katika Jiji la Omsk ilitoa hukumu dhidi ya Ndugu Sergey Polyakov na mke wake, Anastasia, kutia ndani Dada Gaukhar Bektemirova na Dinara Dyusekeyeva.
Ndugu Polyakov alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani. Dada hao watatu walipewa kifungo cha nje cha miaka miwili hadi miwili na nusu na watarudi nyumbani. Alipokuwa akitoa maelezo yake ya mwisho, Ndugu Polyakov alieleza hivi kwa usadikisho: Yesu alitabiri kwamba kwa sababu yake, wafuasi wake watafikishwa mbele ya watawala na wafalme ili kutoa ushahidi. Kwa maoni ya Biblia, kesi hii mahakamani ni utimizo wa unabii, ili wale ambao hawafahamu mamlaka ya Mungu wasikie kuihusu na kujiamulia ikiwa wataikubali au la.—Mathayo 10:18.