Hamia kwenye habari

SEPTEMBA 25, 2020
URUSI

Mahakama ya Urusi Yatoa Hukumu ya Miaka Miwili Dhidi ya Ndugu Konstantin Bazhenov, Mke Wake, na Dada Mwenye Umri wa Miaka 73

Mahakama ya Urusi Yatoa Hukumu ya Miaka Miwili Dhidi ya Ndugu Konstantin Bazhenov, Mke Wake, na Dada Mwenye Umri wa Miaka 73

Septemba 25, 2020, Mahakama ya Wilaya ya Yelizovsky katika Eneo la Kamchatka ilitoa hukumu dhidi ya Ndugu Konstantin Bazhenov, mke wake, Snezhana, na Dada Vera Zolotova. Mwanzoni mwendesha-mashtaka alitaka kuwatoza Ndugu na Dada Bazhenov faini ya rubo 600,000 (dola 7,850 za Marekani) na kumtoza Dada Zolotova faini ya rubo 400,000 (dola 5,195 za Marekani). Hata hivyo, mahakama iliwahukumu kifungo cha nje cha miaka miwili ikifuatiwa na miezi sita ya vizuizi. Ndugu na Dada Bazhenov na Dada Zolotova wanafurahi kwamba hawatahitaji kwenda gerezani wala kulipa faini.