Hamia kwenye habari

Ndugu Yevgeniy Fedin na Sergey Loginov

MEI 2, 2019
URUSI

Mahakama ya Urusi Yawaachilia Huru Ndugu Wawili Waliobaki Mahabusu Huko Surgut

Mahakama ya Urusi Yawaachilia Huru Ndugu Wawili Waliobaki Mahabusu Huko Surgut

Aprili 9, 2019, Mahakama ya Jiji la Surgut iliagiza kwamba Ndugu Yevgeniy Fedin na Sergey Loginov waachiliwe huru. Agizo hilo linapingana na ombi la wenye mamlaka nchini Urusi la kuongeza muda wao wa kubaki mahabusu. Ingawa bado kesi za uhalifu dhidi ya ndugu wote wawili zinachunguzwa, waliruhusiwa kuondoka Aprili 11.

Ndugu Fedin na Loginov walikuwa mahabusu tangu Februari 15, 2019, ambapo walikamatwa baada ya nyumba nyingi kuvamiwa katika jiji la Surgut. Katika kipindi hicho, wenye mamlaka walifungua kesi za uhalifu dhidi ya Mashahidi 19. Watatu kati yao, Yevgeniy na Sergey, pamoja na Ndugu Artur Severinchik, waliamriwa kubaki mahabusu. Artur aliachiliwa Machi 15.

Polisi walipovamia nyumba za Mashahidi mwezi wa Februari, walitesa ndugu saba kati ya waliowakamata, kutia ndani Ndugu Loginov. Malalamiko yametumwa kuhusu jinsi alivyotendewa katika Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu. Malalamiko hayo bado yanachunguzwa.

Tuna uhakika kwamba Yehova ataendelea kuonyesha kwamba anakazia uangalifu sala zetu anapowaimarisha ndugu na dada zetu waaminifu nchini Urusi.—Zaburi 10:17.