Hamia kwenye habari

Kushoto hadi kulia, safu ya juu: Ndugu Aleksey Antyukhin, Ndugu Sergey Baev, Ndugu Yuriy Galka, Ndugu Valeriy Gurskiy, na Ndugu Vitaliy Nerush. Safu ya chini: Ndugu Igor Popov, Ndugu Yevgeniy Sokolov, Ndugu Mikhail Veselov, na Ndugu Anatoliy Yagupov

SEPTEMBA 20, 2022
URUSI

Matokeo Mazuri ya Uvumilivu

Matokeo Mazuri ya Uvumilivu

Mahakama ya Wilaya ya Levoberezhniy iliyo katika Jiji la Voronezh itatangaza hivi karibuni uamuzi wake katika kesi inayowahusu Ndugu Aleksey Antyukhin, Ndugu Sergey Baev, Ndugu Yuriy Galka, Ndugu Valeriy Gurskiy, Ndugu Igor Popov, Ndugu Vitaliy Nerush, Ndugu Stepan Pankratov, a Ndugu Yevgeniy Sokolov, Ndugu Mikhail Veselov, na Ndugu Anatoliy Yagupov. Mwendesha-mashtaka bado hajatoa ombi la hukumu anayopendekeza.

Mfuatano wa Matukio

  1. Julai 13, 2020

    Zaidi ya nyumba 100 za Mashahidi wa Yehova zilizo Voronezh na maeneo ya karibu zilifanyiwa msako. Zaidi ya ndugu na dada 40 walipelekwa kituoni kuhojiwa. Ndugu kumi walioorodheshwa hapo juu waliwekwa kizuizini.

  2. Julai 14-15, 2020

    Ndugu wote kumi walipelekwa mahabusu

  3. Agosti 3–Septemba 18, 2020

    Ndugu Baev, Ndugu Pankratov, Ndugu Popov, na Ndugu Yagupov waliachiliwa kutoka mahabusu na kuwekwa katika kifungo cha nyumbani

  4. Desemba 1-3, 2020

    Ndugu Antyukhin, Ndugu Galka, Ndugu Gurskiy, Ndugu Nerush, Ndugu Sokolov, na Ndugu Veselov waliachiliwa kutoka mahabusu. Ndugu Baev, Ndugu Pankratov, Ndugu Popov na Ndugu Yagupov waliachiliwa kutoka katika kifungo cha nyumbani

  5. Desemba 13, 2021

    Kesi ya uhalifu ilianza

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tunatiwa moyo tunapoona matokeo mazuri ya uvumilivu wa ndugu na dada zetu nchini Urusi kadiri wanavyoendelea kumtegemea Yehova.​—Yakobo 1:4.

a b Hatukuweza kupata picha ya Ndugu Pankratov.