Hamia kwenye habari

Ndugu Aleksandr Lubin na mke wake, Tatyana

FEBRUARI 5, 2024
URUSI

“Mkabidhi Yehova Njia Yako”

“Mkabidhi Yehova Njia Yako”

Mahakama ya Wilaya ya Shadrinskiy iliyo katika Eneo la Kurgan itatangaza uamuzi wake hivi karibuni katika kesi inayomhusu Ndugu Aleksandr Lubin. Mwendesha-mashtaka bado hajatoa ombi la hukumu anayopendekeza.

Maelezo Mafupi Kumhusu

Tuna uhakika kwamba kama Aleksandr, hata iwe tutakabili hali gani, tunaweza kuvumilia majaribu kwa uaminifu huku tukitegemea msaada wa Yehova.​—Isaya 38:14.

Mfuatano wa Matukio

  1. Julai 13, 2021

    Kesi ya uhalifu ilianzishwa

  2. Julai 14, 2021

    Nyumba nane za Mashahidi wa Yehova zilifanyiwa msako. Aleksandr alikamatwa, akahojiwa, na kuwekwa kizuizini

  3. Julai 16, 2021

    Alisafirishwa na kupelekwa mahabusu

  4. Julai 19, 2021

    Alikata rufaa kwa sababu ya hali mbaya ya afya

  5. Agosti 28, 2021

    Baada ya Mahakama ya Umoja wa Ulaya ya Haki za Kibinadamu na mashirika ya haki za binadamu kuomba aachiliwe, Aleksandr aliachiliwa na kuwekewa vizuizi vya kusafiri

  6. Julai 14, 2023

    Kesi ya uhalifu ilianza

  7. Septemba 7, 2023

    Kesi iliahirishwa kwa sababu Aleksandr alikuwa amelazwa