Hamia kwenye habari

Dada Galina Parkova

JANUARI 25, 2021
URUSI

Mume Wake Akiwa Mahabusu, Dada Galina Parkova Anasubiri Kuhukumiwa kwa Sababu ya Imani Yake

Mume Wake Akiwa Mahabusu, Dada Galina Parkova Anasubiri Kuhukumiwa kwa Sababu ya Imani Yake

Hukumu Inatarajiwa

Mahakama ya Wilaya ya Leninskiy katika Eneo la Rostov-on-Don inapanga kutangaza hukumu yake hivi karibuni katika kesi ya Dada Galina Parkova. a Ikiwa atahukumiwa, upande wa mashtaka umeiomba mahakama impe adhabu ya kifungo cha nje cha miaka mitatu.

Maelezo Mafupi Kumhusu

Galina Parkova

  • Alizaliwa: 1970 (Kaltan)

  • Maisha Yake: Mwaka wa 1990, Galina alifunga ndoa na Aleksandr. Wana watoto watatu wa kike na wajukuu wawili. Walifundishwa Biblia na Mashahidi wa Yehova. Alibatizwa mwaka wa 1995. Anapenda kuimba na kuchora

Historia ya Kesi

Juni 6, 2019, wenye mamlaka walifungua kesi ya uhalifu dhidi ya Galina. Majuma kadhaa mapema, mume wake, Aleksandr, alikamatwa na kuwekwa mahabusu.

Kwa kuwa mume wake amefungwa, ni vigumu sana kwa Galina kuwa na pesa za kutosha ili kujitegemeza. Kwa kuongezea, wenye mamlaka wamezuia kadi ya benki ya Galina hivi kwamba ni vigumu kwake kutumia pesa zake, kutia ndani mshahara wake. Hivyo, alilazimika kuacha kazi yake ya awali na sasa anafanya vibarua mbalimbali ili kujiruzuku.

Ndugu na dada zetu nchini Urusi ni “watu waadilifu wanaotendewa kana kwamba walikuwa wametenda uovu.” (Mhubiri 8:14) Hata hivyo, imani yao inatuchochea tuendelee kuwa imara hata tukikabili jaribu gani.

a Tarehe ya hukumu haitangazwi mapema kila mara.