JUNI 30, 2020
URUSI
Mwendesha-Mashtaka Akata Rufaa Uamuzi wa Kumwachilia Mapema Dennis Christensen
Tumepata habari kwamba mwendesha mashtaka, A. A. Shatunov wa Ofisi ya Umma ya Mwendesha-Mashtaka wa Eneo la Kursk, amekata rufaa itakayozuia kuachiliwa huru kwa Ndugu Dennis Christensen. Ingawa mawakili wake watajaza ombi la kuzuia rufaa hiyo, majuma kadhaa yatapita kabla ya mahakama kupanga kusikiliza rufaa hiyo. Gereza limemweka Ndugu Christensen katika jela ya kutia adhabu kwa siku kumi. Licha ya hali hizo, Ndugu Christensen anaendelea vizuri. Asanteni kwa sala mnazoendelea kutoa kwa ajili ya Ndugu na Dada Christensen.