MACHI 1, 2024
URUSI
Ndugu Aleksandr Chagan Amehukumiwa Kifungo cha Miaka Minane Gerezani
Februari 29, 2024, Mahakama ya Wilaya ya Tsentralniy Tolyatti katika Mkoa wa Samara ilimhukumu Ndugu Aleksandr Chagan kifungo cha miaka nane gerezani. Alichukuliwa kutoka katika chumba cha mahakama na kupelekwa gerezani.
Maelezo Mafupi Kumhusu
Tunaendelea kusali kwa Yehova kwamba ‘uso wake umuangazie’ Aleksandr na wote ambao wanaendelea kudumisha bidii kwa ajili ya jina lake.—Zaburi 119:135, 139.
Mfuatano wa Matukio
Machi 4, 2022
Nyumba ilifanyiwa msako
Septemba 14, 2022
Kesi ya uhalifu ilifunguliwa
Septemba 21, 2022
Nyumba ilifanyiwa msako kwa mara ya pili
Septemba 22, 2022
Alihojiwa na kuzuiliwa usiku kucha
Septemba 23, 2022
Aliachiliwa na kuwekewa vizuizi vya kusafiri
Agosti 23, 2023
Kesi ya uhalifu ilianza
Februari 29, 2024
Alihukumiwa kifungo cha miaka nane gerezani
a Maelezo ya Ndugu Chagan yalichukuliwa kabla ya hukumu kutolewa.