Hamia kwenye habari

FEBRUARI 10, 2021
URUSI

Ndugu Aleksandr Ivshin Amehukumiwa Miaka Saba na Nusu Gerezani, Hukumu Kali Zaidi Tangu Marufuku ya 2017

Ndugu Aleksandr Ivshin Amehukumiwa Miaka Saba na Nusu Gerezani, Hukumu Kali Zaidi Tangu Marufuku ya 2017

Februari 10, 2021, Mahakama ya Wilaya ya Abinskiy katika Eneo la Krasnodar, Urusi, ilimhukumu Ndugu Brother Aleksandr Ivshin, mwenye umri wa miaka 63, kifungo cha miaka saba na nusu gerezani. Hiyo ndiyo hukumu kali zaidi kupewa Shahidi wa Yehova tangu tengenezo letu lilipopigwa marufuku mwaka wa 2017.

Ndugu Ivshin alifunguliwa kesi ya uhalifu Aprili 23, 2020. Ameshtakiwa kwa “uhalifu” wa kupanga huduma za kidini kupitia video iliyounganishwa kwenye mtandao na kuimba nyimbo za Ufalme. Wakati wa maelezo yake ya mwisho mahakamani, alionyesha wazi kabisa msingi wa Kimaandiko wa imani yake na kusema: “Mheshimiwa, msimamo wangu maishani unategemea kanuni za Biblia, ambamo hakuna hisia zenye msimamo mkali wala chuki.”