Hamia kwenye habari

Ndugu Aleksey Budenchuk akiwa na Yegor, mwana wake; Sofiya, binti yake; na Tatyana, mke wake

JULAI 7, 2021
URUSI

Ndugu Aleksey Budenchuk Ameachiliwa Kutoka Gerezani Urusi

Ndugu Aleksey Budenchuk Ameachiliwa Kutoka Gerezani Urusi

Julai 6, 2021 Ndugu Aleksey Budenchuk aliachiliwa kutoka gerezani katika jiji la Orenburg baada ya kukamilisha kifungo chake. Yeye ni mmoja kati ya ndugu sita katika jiji la Saratov ambao walifungwa mnamo Septemba 2019. Kwa sasa, watatu bado wako gerezani. Familia na marafiki wa Aleksey walisafiri zaidi ya kilomita 800 ili wawepo anapoachiliwa. Atarudi nyumbani Saratov pamoja na familia yake.