Hamia kwenye habari

Ndugu Andrey Danielyan na mke wake, Nina

NOVEMBA 9, 2022
URUSI

Ndugu Andrey Danielyan Ahukumiwa Miaka Sita Gerezani

Ndugu Andrey Danielyan Ahukumiwa Miaka Sita Gerezani

Novemba 7, 2022, Mahakama ya Jiji la Rubtsovskiy iliyo katika Eneo la Altai ilimhukumu Ndugu Andrey Danielyan kifungo cha miaka sita gerezani. Alipelekwa gerezani moja kwa moja.

Mfuatano wa Matukio

  1. Mei 25, 2021

    Kwa miezi kadhaa, wenye mamlaka walisikiliza kisiri mazungumzo ya Andrey kwenye simu na pia walitumia njia nyingine za kuchunguza utendaji wake, kisha wakaanzisha kesi ya uhalifu dhidi yake

  2. Mei 26, 2021

    Nyumba yake ilifanyiwa msako. Andrey na mke wake walizuiliwa na kuhojiwa. Andrey aliwekewa vizuizi vya kusafiri

  3. Julai 13, 2022

    Alishtakiwa kwa madai ya kupanga utendaji wa shirika lenye msimamo mkali

  4. Septemba 5, 2022

    Kesi ya uhalifu ilianza

  5. Novemba 7, 2022

    Alihukumiwa kifungo cha miaka sita gerezani

Maelezo Mafupi Kumhusu

Tunathamini sana mfano mzuri wa Andrey na ndugu na dada zetu ambao wameazimia kusitawisha ujitoaji-kimungu huku sote tukisubiria kwa hamu ‘ahadi ya uhai utakaokuja.’​—1 Timotheo 4:8.

a Ndugu Danielyan alitoa maelezo haya kabla ya kuhukumiwa.