Hamia kwenye habari

Ndugu Andrey Okhrimchuk

AGOSTI 3, 2021
URUSI

Ndugu Andrey Okhrimchuk Anategemea Nguvu za Yehova

Ndugu Andrey Okhrimchuk Anategemea Nguvu za Yehova

Mfuatano wa Matukio

  1. Oktoba 4, 2021

    Mahakama ya Eneo la Rostov ilikataa ombi la rufaa la Andrey. Hukumu yake ya awali itaendelea kutumika. Hahitaji kwenda gerezani wakati huu

  2. Agosti 2, 2021

    Mahakama ya Wilaya ya Leninskiy iliyoko Rostov-on-Don ilimhukumu Ndugu Andrey Okhrimchuk kifungo cha nje cha miaka minne.

  3. Aprili 5, 2021

    Kesi ya uhalifu ilianza kusikilizwa

  4. Oktoba 29, 2020

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa. Alishtakiwa kushiriki mikutano ya kidini kinyume cha sheria na kuunga mkono utendaji wa shirika lenye msimamo mkali

  5. Mei 22, 2019

    Maofisa wa usalama walifanya upekuzi mapema asubuhi katika nyumba na gari la Andrey

Maelezo Mafupi Kumhusu

Imani yenye nguvu ambayo ndugu na dada zetu nchini Urusi wanaonyesha ni mfano mzuri kwetu sote. Tunajua kwamba Andrey na familia yake watafaulu kuvumilia jaribu hili wanapoendelea kumtegemea Baba yetu wa mbinguni, Yehova.—Zaburi 37:5.