Hamia kwenye habari

Ndugu na Dada Oniszczuk wakiwa wameungana tena katika Mahakama ya Eneo la Kirov

SEPTEMBA 6, 2019
URUSI

Ndugu Andrzej Oniszczuk Aachiliwa Kutoka Gerezani Baada ya Miezi 11 Katika Kifungo cha Upweke

Ndugu Andrzej Oniszczuk Aachiliwa Kutoka Gerezani Baada ya Miezi 11 Katika Kifungo cha Upweke

Mnamo Septemba 3, 2019, Ndugu Andrzej Oniszczuk aliachiliwa kutoka gereza moja nchini Urusi. Alikuwa amefungwa tangu Oktoba 9, 2018, kwa sababu tu ya imani yake. Katika kipindi hicho, aliwekwa katika kifungo cha upweke na hakuruhusiwa kumwona wala kuzungumza na mke wake, Anna. Ingawa ameruhusiwa kurudi nyumbani, bado amewekewa vizuizi ambavyo vinamzuia kusafiri mbali. Bado kesi yake ya mashtaka ya uhalifu inaendelea.

Tunashangilia kwamba Ndugu Andrzej Oniszczuk na mke wake wanadumisha imani thabiti katika kipindi hiki kigumu. Tunashukuru kwamba Yehova anajibu sala zote zinazotolewa kwa ajili ya wale ambao ‘wamefungwa gerezani.’—Wakolosai 4:2, 3.