Hamia kwenye habari

APRILI 8, 2021
URUSI

Ndugu Artur Lokhvitskiy Amepoteza Kesi Yake ya Rufaa

Ndugu Artur Lokhvitskiy Amepoteza Kesi Yake ya Rufaa

Aprili 8, 2021, Mahakama ya Eneo Lililotengewa Wayahudi ilikataa ombi la rufaa la Ndugu Lokhvitskiy. Hukumu yake ya kifungo cha nje cha miaka miwili na miezi sita itaanza kutumika. Hatahitaji kwenda gerezani wakati huu.