Hamia kwenye habari

Kushoto hadi kulia: Ndugu Sergey Britvin na Ndugu Vadim Levchuk wakiwa kizimbani

AGOSTI 20, 2020
URUSI

Ndugu Britvin na Ndugu Levchuk Wanaweza Kufungwa Miaka Sita na Nusu Gerezani Nchini Urusi

Ndugu Britvin na Ndugu Levchuk Wanaweza Kufungwa Miaka Sita na Nusu Gerezani Nchini Urusi

Siku Hukumu Itatangazwa

Hukumu Iliyopendekezwa

Miaka sita na nusu gerezani

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Sergey Britvin

  • Alizaliwa: 1965 (Eneo la Kemerovo)

  • Maisha Yake: Amefanya kazi ya kuendesha kreni na malori kwa miaka mingi. Alistaafu kwa sababu afya yake ilianza kudhoofika. Anafurahia michezo

  • Mwaka 1992, alimwoa Natalya. Alianza kujifunza Biblia mwaka wa 1995 baada ya kujifunza kuhusu ahadi ya Mungu ya ufufuo. Miaka mingi baadaye, Natalya aliamua kujifunza Biblia. Alivutiwa na imani ya Sergey, na alipendezwa kuona jinsi imemchochea kufanya mabadiliko mengi yanayofaa

Vadim Levchuk

  • Alizaliwa: 1972 (Eneo la Kemerovo)

  • Maisha Yake: Alilelewa katika familia ya isiyopendezwa na dini. Alifanya kazi katika mgodi kwa miaka 14

  • Mnamo 1992, alianza kujifunza Biblia. Alimwoa Tatiana mnamo 1997. Ana watoto wawili. Familia yote inaiheshimu Biblia. Pia, wanafurahia michezo mbalimbali

Historia ya Kesi

Julai 22, 2018, maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa (FSB) walivamia nyumba nane za ndugu zetu katika jiji la Berezovsky. Waliwakamata Ndugu Britvin na Ndugu Levchuk na kuwaweka kizuizini ili kuwahoji. Baada ya hilo, Mahakama ya Wilaya ya Kemerovo iliagiza ndugu hao wawili wawekwe mahabusu. Wamekuwa huko kwa karibu mwaka mmoja na nusu. Desemba 25, 2019, waliwekwa katika kifungo cha nyumbani ambacho bado kinaendelea.

Ndugu Britvin na Ndugu Levchuk ni ndugu wawili tu kati ya ndugu watano wanaokabili mashtaka ya uhalifu katika Eneo la Kemerovo kwa sababu ya imani yao. Tunawakumbuka na kusali kwa ajili ya ndugu na dada zetu waliofungwa nchini Urusi. Waebrania 13:3 inatukumbusha hivi: “Wakumbukeni wale walio gerezani, kana kwamba mmefungwa pamoja nao, na wale wanaoteswa, kwa kuwa ninyi pia mko katika mwili.”

a Inaweza kubadilishwa