Hamia kwenye habari

JULAI 11, 2020
URUSI

Ndugu Dennis Christensen Amehamishwa Kutoka Jela ya Adhabu na Kurudishwa Eneo la Kawaida la Wafungwa

Ndugu Dennis Christensen Amehamishwa Kutoka Jela ya Adhabu na Kurudishwa Eneo la Kawaida la Wafungwa

Julai 11, 2020, gereza la Lgov lilimrudisha Ndugu  Dennis Christensen kwenye eneo la kawaida la wafungwa. Alikuwa amepelekwa kwenye jela ya adhabu maalumu, ambako aliwekwa kwa siku 15 zilizopita. Kama ilivyoripotiwa hapo awali, alidhibiwa kwa sababu ya makosa ya uwongo. Sasa yuko pamoja na wafungwa wengine gerezani. Hata hivyo, bado yeye ni mchangamfu. Mawakili wa Ndugu Christensen wanapanga kukata rufaa mashtaka hayo ya karibuni, wakitumaini kwamba mashtaka hayo hayataathiri ombi lake la kuachiliwa mapema.