Hamia kwenye habari

Kushoto hadi kulia: Ndugu Roman Gridasov na mke wake, Elvira, na Ndugu Gennadiy German na mke wake, Nadezhda, muda mfupi baada ya kuachiliwa. Ndugu hawa walikuwa wamefungwa kwa karibu miaka miwili

JULAI 30, 2021
URUSI

Ndugu Gennadiy German na Ndugu Roman Gridasov Wameachiliwa Kutoka Gerezani Urusi

Ndugu Gennadiy German na Ndugu Roman Gridasov Wameachiliwa Kutoka Gerezani Urusi

Julai 29, 2021, Ndugu Gennadiy German na Ndugu Roman Gridasov waliachiliwa huru kutoka gerezani baada ya kukamilisha vifungo vyao. Ndugu hao walikuwa miongoni mwa ndugu watano kutoka Saratov ambao walipigwa baada ya kufikishwa gerezani huko Orenburg. Ndugu Feliks Makhammadiyev aliachiliwa huru Januari 2021 na Ndugu Aleksey Budenchuk akaachiliwa Julai 2021. Ndugu Aleksey Miretskiy ndiye bado amefungwa katika gereza la Orenburg naye anapaswa kuachiliwa mapema mwezi Agosti 2021.