Hamia kwenye habari

Ndugu Gennady Shpakovskiy, akiwa ameachiliwa kutoka gerezani, akipokelewa na mke wake, Tatiana, na binti yao, Maria

AGOSTI 3, 2020
URUSI

Ndugu Gennady Shpakovskiy Ameachiliwa Kutoka Gerezani

Ndugu Gennady Shpakovskiy Ameachiliwa Kutoka Gerezani

Jumatatu, Agosti 3, 2020, Mahakama ya Eneo la Pskov iliamua kumwachilia Ndugu Gennady Shpakovskiy kutoka gerezani. Mahakama ilibadili kifungo chake cha gerezani cha miaka sita na nusu kuwa kifungo cha nyumbani. Muda mfupi baada ya mahakama kufanya uamuzi huo, Ndugu Sphakovskiy aliachiliwa. Mwendesha-mashtaka ana haki ya kukata rufaa.