Hamia kwenye habari

JUNI 9, 2020
URUSI

Ndugu Gennady Shpakovskiy Anakabili Kifungo cha Miaka Saba na Nusu Katika Gereza la Urusi

Ndugu Gennady Shpakovskiy Anakabili Kifungo cha Miaka Saba na Nusu Katika Gereza la Urusi

Jumanne, Juni 9, 2020, Mahakama ya Jiji la Pskov ilimhukumu Ndugu Gennady Shpakovskiy mwenye umri wa miaka 61 kifungo cha miaka sita na nusu gerezani. Alipelekwa gerezani moja kwa moja baada ya kutoka mahakamani. Hiyo ndiyo hukumu ndefu zaidi ambayo ndugu yetu amewahi kupewa tangu uamuzi wa Mahakama Kuu ya Urusi wa mwaka 2017 uliotangaza kazi yetu kuwa ya uhalifu. Ndugu Shpakovskiy atakata rufaa uamuzi wa kumfunga.