Hamia kwenye habari

Ndugu Igor Ivashin

MACHI 27, 2020
URUSI

Ndugu Igor Ivashin Anaweza Kufungwa kwa Miaka Saba Gerezani

Ndugu Igor Ivashin Anaweza Kufungwa kwa Miaka Saba Gerezani

Machi 31,2020, Mahakama ya Wilaya ya Lensky ya Jamhuri ya Sakha itamhukumu Ndugu Igor Ivashin. Mwendesha mashtaka ameiomba mahakama imhukumu kifungo cha miaka saba gerezani.

Februari 2018, Mahakama ya Jiji la Yakutsk iliwaagiza polisi waanze kufuatilia simu alizokuwa akipiga na kupokea. Baada ya miezi kadhaa, polisi walivamia nyumba nane za Mashahidi kutia ndani nyumba ya Ndugu Ivashin. Hivyo,Ndugu Ivashin pamoja na Mashahidi wengine 21 walipelekwa kituoni na kuhojiwa. Mwendesha mashtaka msaidizi alidai kwamba Ndugu Ivashin ndiye aliyekuwa akiandaa shughuli za shirika “lililo na msimamo mkali.”

Novemba 20, 2019, kesi hiyo ilirudishwa kwa mwendesha mashtaka kwa sababu hakukuwa na ushahidi wa kutosha kumfungulia mashtaka hayo mahakamani. Mwendesha mashtaka alikata rufaa, kisha kesi hiyo ikahamishiwa kwenye mahakama ya wilaya. Kesi ilianza kusikilizwa Februari 2020.

Ndugu Ivashin na mke wake, Natalia, wana mabinti wawili. Tunasali kwamba familia ya Ivashin iendelee “[kuvumilia] kikamili kwa subira na shangwe” kesi hii inapokaribia kufika mwisho.—Wakolosai 1:11.