Hamia kwenye habari

Ndugu Igor Tsarev

JANUARI 28, 2021
URUSI

Ndugu Igor Tsarev Anaweza Kufungwa Miaka Minne Gerezani kwa Kujifunza Biblia

Ndugu Igor Tsarev Anaweza Kufungwa Miaka Minne Gerezani kwa Kujifunza Biblia

Hukumu Inatarajiwa

Februari 1, 2021, a Mahakama ya Wilaya ya Birobidzhan katika Eneo Lililotengewa Wayahudi inatarajiwa kutangaza uamuzi katika kesi inayomhusu Ndugu Igor Tsarev. Anaweza kufungwa miaka minne gerezani.

Maelezo Mafupi Kumhusu

Igor Tsarev

  • Alizaliwa: 1974 (Birakan, Eneo Lililotengewa Wayahudi)

  • Maisha Yake: Ana dada wawili. Alipokuwa bado anasoma, alifanya kazi ya kukata miti, useremala, na akiwa fundi umeme ili kuitegemeza familia yake. Anapenda kuvua samaki na kufurahia mazingira

  • Alianza kufikiria kuhusu kusudi la uhai alipokuwa anatumikia jeshini. Uchunguzi wao ulimfanya yeye na baba yake waanze kujifunza Biblia. Alibatizwa mwaka wa 1997. Alifunga ndoa na Viktoriya, mwaka wa 1998. Wana binti mmoja mdogo

Historia ya Kesi

Julai 30, 2019, wenye mamlaka nchini Urusi walifungua kesi ya uhalifu dhidi ya Ndugu Igor Tsarev. Anashtakiwa kwa kosa la kujifunza Biblia “ili kuwafundisha watu mafundisho ya Mashahidi wa Yehova.” Rekodi za video zilizorekodiwa kwa siri na maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa (FSB), zimetumiwa kama ushahidi dhidi ya Igor. Katika hali isiyo ya kawaida, mwendesha-mashtaka aliomba kwamba kesi iendeshwe bila watazamaji. Mwendesha-mashtaka alisema hilo ni muhimu ili wasikilizaji wasishawishiwe na mambo ambayo Igor anaamini. Ombi hilo lilikubaliwa.

Igor anasema hivi: “Hivi karibuni, uamuzi wa mahakama utabadili kabisa maisha yangu. Kwa kweli, maisha yangu tayari yamebadilika. Niko chini ya dhamana inayoninyima uhuru wa kusafiri. Nimelazimika kumweleza mwajiri wangu kwa nini vyombo vya usalama vinanichunguza. Imekuwa vigumu kwa mwajiri wangu na wafanyakazi wenzangu kuelewa kwa nini nimeshtakiwa, hata hivyo wanakiri kwamba sikuzote Wakristo wamekuwa wakinyanyaswa.”

Tunasali kwa niaba ya Igor na familia yake. Tunajua kwamba Yehova atawapatia “nguvu kupitia roho yake.”—Waefeso 3:16.

a Huenda Itabadilika.