Hamia kwenye habari

Ndugu Konstantin Bazhenov akionana na mke wake, Irina kifupi, baada tu ya kuachiliwa huru kutoka gerezani. Kwa sasa yuko mahabusu akisubiria kusafirishwa

MEI 5, 2021
URUSI

Ndugu Konstantin Bazhenov Ameachiliwa Kutoka Gerezani Urusi, Anasubiri Kupelekwa Uhamishoni Ukrainia

Ndugu Konstantin Bazhenov Ameachiliwa Kutoka Gerezani Urusi, Anasubiri Kupelekwa Uhamishoni Ukrainia

Mei 5, 2021, Ndugu Konstantin Bazhenov alikamilisha kifungo chake na kuachiliwa kutoka kwenye gereza la Dimitrovgrad. Kwa kuwa uraia wake wa Urusi ulifutwa mnamo Mei 2020, Konstantin alipelekwa moja kwa moja kwenye kituo cha kuwazuilia raia wa kigeni wanaosubiri uhamisho. Atapelekwa uhamishoni nchini Ukrainia hivi karibuni.