Hamia kwenye habari

FEBRUARI 11, 2020
URUSI

Ndugu Mikhail Popov na Mke Wake, Yelena, Wanakabiliwa na Mashtaka Katika Mahakama ya Urusi—Uamuzi Watarajiwa Kutolewa Februari 13, 2020

Ndugu Mikhail Popov na Mke Wake, Yelena, Wanakabiliwa na Mashtaka Katika Mahakama ya Urusi—Uamuzi Watarajiwa Kutolewa Februari 13, 2020

Februari 13, 2020, Mahakama ya Jiji ya Vilyuchinsk yatarajiwa kutangaza uamuzi wake katika kesi inayomhusu Ndugu Mikhail Popov na mke wake, Dada Yelena Popova. Wenzi hao wa ndoa walikamatwa Julai 30, 2018, huko Kamchatka kisha waliachiliwa Agosti 9, 2018. Wameshtakiwa kushiriki “utendaji wenye msimamo mkali.”

Mikhail na Yelena wanamtegemea Yehova wanapoendelea kukabiliana na hali hii ngumu.Tuna hakika kwamba Yehova ataendelea kuwa ‘kimbilio lao na nguvu zao’—Zaburi 46:1.