Hamia kwenye habari

Ndugu Nikolay Voishchev

SEPTEMBA 27, 2023
URUSI

Ndugu Nikolay Voishchev Ahukumiwa Kifungo cha Miaka Mitatu Gerezani

Ndugu Nikolay Voishchev Ahukumiwa Kifungo cha Miaka Mitatu Gerezani

Septemba 14, 2023, Mahakama ya Jiji la Maykop iliyo katika Jamhuri ya Adygeya ilimhukumu Ndugu Nikolay Voishchev kifungo cha miaka mitatu gerezani. Amekuwa mahabusu tangu Oktoba 20, 2022, na ataendelea kubaki gerezani.

Maelezo Mafupi Kumhusu

Tunasikitishwa sana kusikia kwamba Nikolay atafungwa gerezani, hata hivyo, tuna uhakika kwamba Yehova ataendelea kumfariji na kumpa nguvu, pamoja na ndugu na dada zetu wote wanaokabili majaribu.​—Zaburi 119:76.

Mfuatano wa Matukio

  1. Oktoba 19, 2022

    Kesi ya uhalifu yafunguliwa

  2. Oktoba 20, 2022

    Nyumba yake ilifanyiwa msako. Nikolay alihojiwa na kuwekwa kizuizini

  3. Oktoba 21, 2022

    Alihamishiwa mahabusu

  4. Januari 11, 2023

    Hakimu aliombwa amruhusu Nikolay kutumikia kifungo cha nyumbani badala ya kuwa mahabusu kwa sababu ya matatizo ya kiafya. Hakimu alikataa ombi hilo na badala yake akamwongezea Nikolay muda wa kukaa mahabusu

  5. Januari 25, 2023

    Kesi ya uhalifu ilianza

  6. Septemba 14, 2023

    Alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani

a Kwa kuwa Ndugu Voishchev alikuwa mahabusu, hatukuweza kupata maelezo kutoka kwake.