Hamia kwenye habari

MEI 25, 2021
URUSI

Ndugu Roman Baranovskiy na Mama Yake, Dada Valentina Baranovskaya, Wamepoteza Rufaa

Ndugu Roman Baranovskiy na Mama Yake, Dada Valentina Baranovskaya, Wamepoteza Rufaa

Mei 24, 2021, Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Khakassia, Urusi, ilikataa ombi la rufaa la Ndugu Baranovskiy na la mama yake mwenye umri wa miaka 70, Dada Valentina Baranovskaya. Watabaki gerezani. Mbali na hilo mahakama iliongezea kwenye hukumu yao kwa kusema kwamba wawekewe vizuizi vya ziada baada ya kuachiliwa kutoka gerezani wakati ujao.