Hamia kwenye habari

Ndugu Semyon Baybak

NOVEMBA 25, 2020
URUSI

Ndugu Semyon Baybak Atafikishwa Mbele ya Mahakama ya Uhalifu kwa Sababu ya Imani Yake

Ndugu Semyon Baybak Atafikishwa Mbele ya Mahakama ya Uhalifu kwa Sababu ya Imani Yake

Hukumu Inatarajiwa

Desemba 18, 2020, a Mahakama ya Wilaya ya Leninskiy katika eneo la Rostov-on-Don inatarajiwa kutangaza uamuzi wake katika kesi inayomhusu Ndugu Semyon Baybak ambaye ni kijana. Mwendesha-mashtaka aliiomba mahakama kwamba Semyon apewe kifungo cha nje cha miaka minne

Maelezo Mafupi Kumhusu

Semyon Baybak

  • Alizaliwa: 1997 (Rostov-on-Don)

  • Maisha Yake: Ana ndugu na dada wenye umri mkubwa kuliko yeye. Alijifunza Kichina na ni mwalimu wa Kichina. Anafurahia kusoma na kuandika mashairi

  • Alifundishwa na wazazi wake kumhusu Yehova alipokuwa mchanga. Alipokuwa akikua alithamini hekima ya ushauri wa Biblia. Imani ilimwongoza kukataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri. Alifanya utumishi wa badala wa kiraia kuanzia 2015 hadi 2017, akifanya kazi ya usafi katika hospitali ya watoto katika eneo lao

Historia ya Kesi

Mei 22, 2019, maofisa kutoka kwenye kituo cha kupambana na ugaidi walishambulia nyumba 13 zaa Mashahidi katika eneo la Rostov-on-Don. Juni 6, 2019, majuma mawili hivi baadaye, Semyon alifunguliwa kesi ya uhalifu. Baada ya hapo, alikamatwa na akawekwa mahabusu kwa siku moja kabla ya mahakama kumpa kifungo cha nyumbani. Mwanzoni kifungo hicho kilikuwa cha majuma manane, lakini kimeongezwa mara saba.

Mwanzoni wenye mamlaka walimshtaki Seymon kwa “makosa” ya kushiriki katika mikutano ya kidini na kuwaeleza wengine mambo aliyojifunza katika Biblia. Novemba 2019, wenye mamlaka walimshtaki kwa kuchangia shirika “lenye msimamo mkali.”

Kadiri mateso hayo yanavyoendelea dhidi ya ndugu na dada zetu nchini Urusi, tunajua kwamba Yehova, yule “Mungu wa amani,” ataendelea kuwapa kila kitu wanachohitaji ‘ili wafanye mapenzi yake.’—Waebrania 13:20, 21.

a Inaweza kubadilishwa.