Hamia kwenye habari

SEPTEMBA 2, 2020
URUSI

Ndugu Sergey Britvin na Vadim Levchuk Wamehukumiwa Kifungo cha Miaka Minne Gerezani Urusi

Ndugu Sergey Britvin na Vadim Levchuk Wamehukumiwa Kifungo cha Miaka Minne Gerezani Urusi

Septemba 2, 2020, Mahakama ya Jiji la Berezovsky katika Eneo la Kemerovo iliwahukumu Ndugu Sergey Britvin na Vadim Levchuk kifungo cha miaka minne gerezani. Mwendesha-mashtaka alikuwa ameiomba mahakama iwafunge kifungo cha miaka sita na nusu. Akina ndugu watakata rufaa uamuzi huo.