Hamia kwenye habari

Ndugu Sergey Gromov na mke wake, Yelena

SEPTEMBA 15, 2023
URUSI

Ndugu Sergey Gromov Ahukumiwa Miaka Sita na Mwezi Mmoja Gerezani Urusi

Ndugu Sergey Gromov Ahukumiwa Miaka Sita na Mwezi Mmoja Gerezani Urusi

Septemba 14, 2023, Mahakama ya Wilaya ya Moskovskiy iliyoko Kazan ilimhukumu Ndugu Sergey Gromov kifungo cha miaka sita na mwezi mmoja gerezani. Amekuwa kizuizini tangu Machi 15, 2022, hivyo atabaki huko.

Maelezo Mafupi Kumhusu

Tunathamini sana jinsi Sergey na Yelena wanaendelea kutuwekea mfano mzuri wa ushikamanifu na kumtegemea Yehova. Tunapojionea uaminifu wao na jinsi Yehova anavyowabariki, tunapata usadikisho wenye nguvu kwamba “mkono wa Yehova si mfupi usiweze kuokoa, wala sikio lake si zito lisiweze kusikia.”​—Isaya 59:1.

Mfuatano wa Matukio

  1. Machi 15, 2022

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa. Alikamatwa akahojiwe na akapelekwa kizuizini

  2. Machi 16, 2022

    Nyumba ilifanyiwa upekuzi

  3. Machi 17, 2022

    Alihamishiwa mahabusu

  4. Machi 30, 2023

    Kesi ya uhalifu ilianza

  5. Septemba 14, 2023

    Alihukumiwa kifungo cha miaka sita na mwezi mmoja gerezani

a Ndugu Gromov alikuwa mahabusu makala hii ilipokuwa ikitayarishwa. Hatukuweza kupata maelezo yake ya kibinafsi.