Hamia kwenye habari

Ndugu Sergey Polyakov akiwa pamoja na mke wake, Anastasia

DESEMBA 7, 2022
URUSI

Ndugu Sergey Polyakov Aachiliwa Huru Nchini Urusi

Ndugu Sergey Polyakov Aachiliwa Huru Nchini Urusi

Novemba 30, 2022, Ndugu Sergey Polyakov aliachiliwa huru kutoka gerezani baada ya kumaliza kifungo chake cha miaka mitatu. Alikamatwa Julai 4, 2018, alifugwa katika vifungo mbalimbali kutia ndani kifungo cha upweke cha miezi mitano.

Sergey alikuwa gerezani kwa miezi 16 katika penal colony iliyo jijini Valday, ni kilometa 3,000 hivi kutoka anakoishi. Alijulikana kuwa mfungwa mwenye imani kubwa na hilo lilifanya aheshimiwe na wasimamizi wa gereza na pia wafungwa wenzake. Alipokuwa gerezani, Sergey alitiwa moyo kupitia barua nyingi alizopokea kutoka kwa familia na marafiki wake. Mara nyingi, alipokea barua nyingi kwa siku hivi kwamba idadi ya barua walizoletewa wafugwa wengine 250 hivi zikijumuishwa pamoja, hazikufikia idadi ya barua alizopokea yeye.

Siku aliyoachiliwa huru, Sergey aliungana na mke wake, Anastasia. Anastasia alifungwa pia kifungo cha miezi mitano cha upweke. Baada ya hapo, alihukumiwa kifungo cha nje kwa sababu ya imani yake. Sergey na mke wake walikuwa wenzi wa ndoa wa kwanza kufungwa baada ya uamuzi uliotangazwa na Mahakama Kuu mwaka wa 2017 wa kwamba utendaji wa Mashahidi wa Yehova unaenda kinyume na sheria.

Zaidi ya ndugu na dada 100 wanaendelea kutumikia vifungo vya gerezani Urusi na Crimea. Tuna uhakika kwamba Yehova ataendelea kuwategemeza wale “[wanaovumilia] taabu na kuteseka isivyo haki kwa sababu ya dhamiri kwa Mungu.”​—1 Petro 2:19.