Hamia kwenye habari

Kushoto: Ndugu Aleksandr Skvortsov. Kulia: Ndugu Valeriy Tibiy

JUNI 27, 2023
URUSI

Ndugu Skvortsov na Ndugu Tibiy Wahukumiwa

Ndugu Skvortsov na Ndugu Tibiy Wahukumiwa

Juni 20, 2023, Mahakama ya Jiji la Taganrog iliyo katika Eneo la Rostov ilimhukumu Ndugu Aleksandr Skvortsov na Ndugu Valeriy Tibiy. Aleksandr alipewa kifungo cha miaka saba gerezani. Amekuwa mahabusu tangu Desemba 7, 2021 kwa hiyo atabaki kizuizini. Valeriy alipewa kifungo cha nje cha miaka sita. Alikuwa kizuizini tangu Mei 18, 2022 hivyo aliachiliwa ili aanze kifungo cha nje.

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tunamshukuru Yehova kwa kututunza kwa upendo na kutupa mwongozo kwa kuwa mambo hayo yanatusaidia kuvumilia jaribu lolote linaloweza kutupata.​—Zaburi 5:12.

Mfuatano wa Matukio

  1. Machi 20, 2021

    Nyumba ya Skvortsov ilifanyiwa msako

  2. Desemba 7, 2021

    Nyumba ya Skvortsov ilifanyiwa msako kwa mara ya pili, siku ambayo nyumba nyingine 29 za Mashahidi wa Yehova jijini Taganrog. Alishtakiwa kuwa mhalifu na kuwekwa kizuizini

  3. Desemba 8, 2021

    Aleksandr aliwekwa mahabusu

  4. Machi 29, 2022

    Kesi ya uhalifu dhidi ya Valeriy ilianza

  5. Machi 31, 2022

    Wapelelezi waliunganisha kesi ya Aleksandr na Valeriy

  6. Mei 18, 2022

    Valeriy alikamatwa na kuwekwa kizuizini

  7. Mei 26, 2022

    Valeriy alikamatwa na kuwekwa mahabusu

  8. Dedemba 6, 2022654

    Kesi ya uhalifu ilianza

  9. Juni 20, 2023

    Aleksandr alihukumiwa kifungo cha miaka saba gerezani. Valeriy alihukumiwa kifungo cha nje cha miaka sita

a b Makala hii ilipokuwa ikitayarishwa, Ndugu Skvortsov na Ndugu Tibiy walikuwa kizuizini hivyo hatukuweza kupata maelezo kutoka kwao.