Hamia kwenye habari

Kulia kwenda kushoto: Ndugu Nikolay Polevodov na Ndugu  Stanislav Kim wakiwa nje ya mlango wa chumba cha Mahakama Oktoba 2019

JANUARI 31, 2020
URUSI

Ndugu Stanislav Kim na Ndugu Nikolay Polevodov Wanakabiliwa na Mashtaka Katika Mahakama Mbili Nchini Urusi, Hukumu ya Kwanza Inatarajiwa Februari 4, 2020

Ndugu Stanislav Kim na Ndugu Nikolay Polevodov Wanakabiliwa na Mashtaka Katika Mahakama Mbili Nchini Urusi, Hukumu ya Kwanza Inatarajiwa Februari 4, 2020

Februari 4, 2020, Mahakama ya Zheleznodorozhniy iliyo katika mji wa Khabarovsk, nchini Urusi inatarajiwa kutangaza hukumu ya kesi inayomhusu Ndugu Stanislav Kim na Ndugu Nikolay Polevodov. Mwendesha mashtaka ameomba ndugu wote wawili wafungwe miaka mitatu katika gereza lenye kambi ya kazi . Hata hivyo, ndugu hao wawili wana kesi nyingine ya uhalifu inayoendelea katika Mahakama ya Wilaya ya Viwanda iliyo katika jiji hilo.

Ndugu Kim na Ndugu Polevodov walikamatwa Novemba 10, 2018. Siku hiyo, karibu ndugu na dada 50 walikusanyika kwenye mkahawa waliokodi jijini Khabarovsk kwa ajili ya kupata vinywaji na programu yenye kuburudisha. Mkutano huo haukuwa wa kidini. Mara tu baada ya kukutana, polisi wengi walikuja pamoja na washiriki wa kamati ya uchunguzi wa jiji hilo na kuvamia mkahawa huo, kisha wakawakamata ndugu na dada hao. Ndugu Kim, Ndugu Polevodov na Ndugu Vitaliy Zhuk waliwekwa mahabusu kwa zaidi ya miezi miwili kisha wakaachiliwa ili kuendelea na kifungo cha nyumbani kwa miezi kadhaa.

Uamuzi uliotolewa Februari 4 ulihusu kesi dhidi ya Ndugu Kim na Ndugu Polevodov tu, wanaotuhumiwa kwa kosa la kushiriki programu hiyo. Hata hivyo, wenye mamlaka wamefungua kesi nyingine dhidi ya Ndugu Kim, Ndugu Polevodov na Ndugu Zhuk pamoja na dada wengine watatu waliohudhuria programu hiyo. Katika kesi hii, Ndugu Kim na Ndugu Polevodov wanashtakiwa kwa kosa la kuandaa tafrija hiyo. Bado tarehe ya hukumu kutolewa haijatangazwa.

Ndugu Kim na Ndugu Polevodov wanakabili hali isiyo ya kawaida kwa kuwa wameshtakiwa kwa kosa la uhalifu katika kesi mbili tofauti kwa wakati huohuo. Wachunguzi wameamua kutounganisha kesi hizo mbili, hivyo inabidi Ndugu Kim na Ndugu Polevodov wahudhurie kesi mbili tofauti katika mahakama mbili tofauti za mkoa wa Khabarovsk.

Ndugu wote wawili wameoa na wana watoto wanaoishi nyumbani. Tunajua kwamba Yehova ataendelea kuwapa ndugu zetu na familia zao roho takatifu na kulinda mioyo yao na nguvu zao za akili, ili waweze kuendelea kuwa waaminifu chini ya majaribu.—Wafilipi 4:7.