Hamia kwenye habari

Dada Tatyana Alushkina akimkumbatia mume wake, Vladimir baada ya kuachiliwa kutoka gerezani

APRILI 10, 2020
URUSI

Ndugu Vladimir Alushkin Aachiliwa Kutoka Gerezani

Ndugu Vladimir Alushkin Aachiliwa Kutoka Gerezani

Machi 30, 2020, Ndugu Vladimir Alushkin aliachiliwa kutoka gerezani na kuungana na mke wake tena.

Aliachiliwa baada ya uamuzi uliofanywa na Mahakama ya Mkoa wa Penza wa Machi 25, uamuzi ambao uliripotiwa awali. Uamuzi huo ulibadilisha hukumu iliyofanywa awali na Mahakama dhidi ya Ndugu Vladimir Alushkin, Vladimir Kulyasov, Andrey Magliv, na Denis Timoshin, pamoja na Dada Tatyana Alushkina na Galiya Olkhova. Mahakama ya Mkoa wa Penza ilirudisha kesi hiyo katika Mahakama iliyoisimamia awali lakini ikasikilizwa na hakimu tofauti. Kwa sasa ndugu na dada hao wote sita wako chini ya vizuizi mbalimbali ikiwemo kizuizi cha kusafiri.

Ingawa tunafurahi kusikia kwamba Ndugu Alushkin ameachiliwa, inasikitisha kwamba siku mbili tu baada ya uamuzi huo, ndugu yetu mwingine alihukumiwa kwa sababu ya imani yake huko kaskazini-mashariki mwa Urusi. Kadiri mashambulizi hayo yasiyo na msingi yanavyoendelea dhidi ya ndugu na dada zetu nchini Urusi, tunajua kwamba wataendelea kukumbuka maneno ya Nahumu 1:7: “Yehova ni mwema, ni ngome katika siku ya taabu. Anawakazia fikira wale wanaotafuta kimbilio kwake.”