Hamia kwenye habari

Ndugu Vladimir Alushkin akiwa na mke wake, Tatyana

SEPTEMBA 16, 2020
URUSI

Ndugu Vladimir Alushkin Hatahitaji Kurudi Gerezani

Ndugu Vladimir Alushkin Hatahitaji Kurudi Gerezani

Septemba 16, 2020, Mahakama ya Eneo la Penza ilitangaza uamuzi wake katika kesi ya rufaa kumhusu Vladimir Alushkin, Vladimir Kulyasov, Andrey Magliv, na Denis Timoshin, pamoja na Dada Tatyana Alushkina na Galiya Olkhova. Mahakama ilipunguza hukumu ya awali kwamba Ndugu Alushkin afungwe miaka sita gerezani na sasa atafungwa kifungo cha nje cha miaka minne. Tunafurahi kwamba hatahitaji kurudi gerezani. Uamuzi wa vifungo vya nje vya wengine wote havijabadilishwa.