DESEMBA 25, 2023
URUSI
Ndugu Vladimir Balabkin Mwenye Umri wa Miaka Sabini na Moja Aachiliwa Kutoka Gerezani
Desemba 19, 2023, Ndugu Vladimir Balabkin aliachiliwa kutoka gerezani baada ya kutumikia sehemu ya kifungo chake cha miaka minne gerezani. Amekuwa gerezani kwa miezi mitatu hivi. Septemba 13, 2023 alihukumiwa kifungo cha gerezani na Vladimir alikata rufaa. Mahakimu watatu waliosikiliza kesi hiyo ya rufaa walibadili hukumu iliyotolewa awali. Hivyo, adhabu yake ilipungua kutoka kifungo cha miaka minne gerezani hadi kifungo cha nje cha mwaka mmoja.
Vladimir alisema hivi kwa ujasiri kesi yake ya uhalifu iliposikilizwa: “Imani yangu inategemea Neno la Mungu, Biblia. Biblia imenisaidia kusitawisha sifa ambazo Muumba anataka watu wawe nazo kama vile upole, fadhili, subira, na sifa ya kujizuia. Sifa hizi zimeninufaisha mimi pamoja na familia yangu. Ninatamani kila mtu alifahamu Neno la Mungu vizuri kwa sababu linaweza kubadili maisha ya mtu na kuyafanya bora zaidi.”
Tunashangilia pamoja na Vladimir na familia yake huku tukiendelea kuwakumbuka wale walio gerezani, nasi tuna uhakika kwamba Yehova atawathawabisha.—Waebrania 10:34.