Hamia kwenye habari

Ndugu Vladimir Filippov pamoja na mke wake, Lyubov

JANUARI 26, 2021
URUSI

Ndugu Vladimir Filippov Mwenye Umri wa Miaka Sabini na Saba Anakabili Kifungo cha Miaka Sita na Nusu Gerezani

Ndugu Vladimir Filippov Mwenye Umri wa Miaka Sabini na Saba Anakabili Kifungo cha Miaka Sita na Nusu Gerezani

Hukumu Inatarajiwa

Januari 27, 2021, a Mahakama ya Wilaya ya Nadezhdinskiy katika Eneo la Primorye, inatarajiwa kutangaza uamuzi wake katika kesi ya Ndugu Vladimir Filippov. Anakabili kifungo cha miaka sita na nusu gerezani.

Maelezo Mafupi Kumhusu

Vladimir Filippov

  • Alizaliwa: 1943 (Oktyabrskiy, Eneo la Novosibirsk)

  • Maisha Yake: Muda mfupi tu kabla hajazaliwa, baba yake alikufa wakati wa Vita vya Pili vya Ulimwengu. Alihitimu kutoka Shule ya Kijeshi ya Tomsk mwaka wa 1964 na kuwa luteni. Mwaka wa 1967 alifunga ndoa na Lyubov. Alitumikia katika jeshi kwa miaka 27 kabla ya kustaafu

    Alianza kujifunza Biblia muda mfupi tu baada ya mke wake kuanza kujifunza mwaka wa 1994. Walibatizwa mwaka uliofuata

Historia ya Kesi

Agosti 2017, wenye mamlaka walianza kurekodi kwa siri video na mazungumzo ya Ndugu Filippov na ndugu wengine katika Razdolnoye. Kwa miezi kadhaa, wenye mamlaka walimrekodi kwa siri Vladimiri akizungumza kwenye mikutano na pia akizungumza na jirani zake kuhusu Biblia.

Julai 19, 2018, maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa (FSB) waliokuwa na silaha na walioficha nyuso zao, walivamia nyumba ya Filippov. Maofisa wa FSB walimpiga Vladimir ngumi usoni, ingawa alikuwa na umri wa miaka 75, wakamlazimisha alale sakafuni, wakamfunga mikono yake mgongoni, na kupekua nyumba yake. Nyumba ya Filippov ilivamiwa mara mbili zaidi mnamo Agosti 2019 na Januari 2020. Baada ya msako wa pili, Vladimir alifunguliwa mashtaka ya uhalifu.

Yehova na aendelee kuwapa ndugu na dada zetu nguvu na uwezo wanaohitaji ili kudumisha imani na shangwe yao!—Isaya 40:29, 31.

a Inaweza kubadilishwa.