Hamia kwenye habari

Safu ya juu, kushoto hadi kulia: Ndugu Aleksey Bogatov, Ndugu Yevgeniy Fomashin, na Ndugu Vladimir Mavrin

Safu ya chini, kushoto hadi kulia: Ndugu Andrey Murych na Ndugu Sergey Tyurin

NOVEMBA 29, 2023
URUSI

Ndugu Watano Nchini Urusi Wahukumiwa Katika Eneo la Saratov

Ndugu Watano Nchini Urusi Wahukumiwa Katika Eneo la Saratov

Novemba 23, 2023, Mahakama ya Wilaya ya Balakovskiy iliyo katika Eneo la Saratov ilitangaza uamuzi wake katika kesi inayowahusu Ndugu Aleksey Bogatov, Ndugu Yevgeniy Fomashin, Ndugu Vladimir Mavrin, Ndugu Andrey Murych, na Ndugu Sergey Tyurin. Ndugu wote watano walitangazwa kuwa na hatia. Aleksey na Vladimir walihukumiwa kifungo cha nyumbani cha miaka sita kila mmoja wao. Andrey, Sergey, na Yevgeniy walitozwa faini ya rubo 300,000 (dola 3,362 za Marekani). Wote hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Mifano ya uaminifu ya ndugu hawa watano inatukumbusha kwamba tunaweza kuvumilia magumu kwa ajili ya habari njema tunapotegemea nguvu za Mungu.​—2 Timotheo 1:8.

Mfuatano wa Matukio

  1. Februari 11, 2022

    Kesi ya uhalifu ilianzishwa

  2. Machi 23, 2022

    Maofisa wa FSB walifanya msako kwenye nyumba za ndugu hao watano. Kila mmoja alihojiwa na kuzuiliwa katika eneo la muda

  3. Machi 25, 2022

    Ndugu hao waliwekwa mahabusu

  4. Januari 23, 2023

    Ndugu hao waliachiliwa kutoka mahabusu na wakawekewa vizuizi vya kusafiri

  5. Julai 21, 2023

    Kesi ya uhalifu ilianza

  6. Novemba 23, 2023

    Hukumu ilitolewa